.

2/14/2019

Kesi ya Zitto dhidi ya Spika na sakata la CAG kuendelea leo


Kesi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kuomba tafsiri ya mahakama kuhusu madaraka ya Bunge kumuita na kumuhoji Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itaendelea leo February 14, 2019 katika Mahakama Kuu.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 01/2019 imefunguliwa Mahakama Kuu, Masjala Kuu na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika.

Zitto Kabwe ameiomba mahakama itoe tafsiri ya kinga ya CAG iliyopo kikatiba na tafsiri ya sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge katika kushtaki wanaodaiwa kulidhalilisha Bunge.