Kiongozi wa Rastafarian kujengewa sanamu makao makuu ya AU

Sanamu ya mfalme wa mwisho wa Ethiopia itajengwa nje ya makao makuu ya muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

Lengo la sanamu hiyo kujengwa nje ya makao hayo ni kutambua mchango wake katika uanzishaji wa OAU ambalo ndio mtangulizi wa Muungao huo wa Afrika.

Lakini huenda hilo sio jambo la kwanza linalokuja katika fikra unaposikia jina Haile Sellasie. Jina hilo linahusishwa sana na mwanamuziki wa Jamaica Bob Marley na Rastafarians.

Hivyobasi ni nani haswa Haile Selassie na ni vipi alianza kuabudiwa kama mungu na watu wanaoishi mbali?.

Haile Selassie alikuwa katika uongozi wake kwa takriban miaka 30 wakati aliposaidia kuanzisha OAU.

Mkutano wake wa kwanza mnamo mwezi Mei 1963 ulifanyika mjini Addis Ababa.

Ethioipia ambayo haijatawaliwa licha ya kuongozwa kijeshi na Itali kwa miaka mitano imeonekana kuwa ishara ya Uhuru wa Afrika tangu kipindi cha ukoloni.

Mataifa mengine yalikuwa yakipata uhuru wao na ikawa fursa ya kuyaunganisha pamoja ili kukabiliana na ukoloni na uongozi wa weupe walio wachache mbali na kushirikisha juhudi za kuinua hali ya maisha na kutetea uhuru wao.

''Ningependa mkutano huu wa Muungano kuwepo kwa miaka 1000'', Selassie, ambaye alitumia mwaka mmoja akiandaa mji huo kwa mkutano huo aliambia wajumbe.

Kama ilivyokuwa OAU ilibadilika na kuwa AU mwaka 2002.

Lakini mchango wake katika kuanzisha muungano huo haujasahaulika , na sanamu hiyo ni njia moja ya AU kutambua mchango wa Selassie.