Kocha wa Yanga SC aukubali uwezo wa mchezaji huyu


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa wachezaji wake wote wanajuhudi Uwanjani na anawapenda ila anakubali uwezo wa chipukizi mmoja anayekuja kwa kasi.

Kocha huyo amesema anakuwa na wachezaji muda mwingi hasa kwenye mazoezi pamoja na mechi ila anakubali zaidi uwezo wa Boxer ambaye ni beki kwenye kikosi cha kwanza.

"Wote wachezaji wazuri na ninawapenda ila ninavutiwa na uwezo wa Paul Godfery, huyu bado kijana na anajuhudi akiwa Uwanjani, naamini  atakuja kufanya mambo makubwa zaidi hapo baadaye iwapo ataendela kufuata maelekezo na kujituma kila siku," amesema Zahera

Boxer alikuwa anachezea Yanga B alipandishwa kikosi cha kwanza baada ya Juma Abdul ambaye ni nahodha msaidizi kupata majeraha licha ya kurejea kwenye kikosi bado Boxer ameendelea kuaminiwa na Zahera.