Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti


Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti.

Kulingana na shirika la habari la BBC,wataalamu wa chuo kikuu cha Bristol nchini Uingereza wamewafanyia tathmini wanawake 400,000 na kutambua kuwa sio rahisi kwa mwanamke anaeamka asubuhi na mapema kupata saratani ya matiti.

Utafiti huo umeoneysha kuwa wanawake wanaoamka wamechelewa wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo ukilinganisha na wale wanaoamka wamechelewa.

Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa kufanya kazi mpaka usiku wa manane kunaongeza hatari ya kupata  saratani.

Matokeo ya utafiti huo yatawasilishwa kwenye Mkutano wa Taifa wa Taasisi ya Utafiti wa Saratani huko Glasgow.