.

2/12/2019

Kwenye mechi za kimataifa nipo na Simba SC asilimia zote - Dkt. Mwigulu


Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaita mashabiki wa soka
nchini kuiuga mkono Simba SC kwenye michezo yake ya kimataifa kwani inapofanya vizuri
inakuwa na faida kwa taifa.

Dkt. Mwigulu amesema kuwa Simba SC itakapofanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika itapelekea nchi kuongezewa idadi ya timu kwenye michuano hiyo.

"Mimi kwenye mechi za kimataifa nipo na Simba kwa asilimia zote, na ninawatakiwa kila la
kheri," amesema.

"Timu mojawapo kama Simba hivi, ikifanya vizuri kwenye mashindano haya, itasababisha nchi yetu
iongezewe nafasi. Mathalani Simba ikafika nusu fainali, msimu ujao nchi yetu inaweza ikapewa nafasi ya timu nne," amesema Dkt. Mwigulu.

Simba SC leo itashuka kwenye dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam kuivaa timu ya Al kutoka nchini Misri. Mchezo wa awali timu hizo kukutana, Simba ilijikuta ikipoteza kwa kuzabwa magoli 5-0.