Lissu anachokiongea hata mtoto mdogo anajua ni uongo - DC Kigamboni


Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,  Bi. Sara Msafiri amesema kuwa vitu anavyoviongea Tundu Lissu katika mahojiano yake  hata mtoto mdogo anajua ni vya uongo.

Akiongea na Muungwana Tv, Bi Sara amesema kuwa inaonekana Mbunge huyo bado anaumwa huku akieleza kuwa suala lake halihitaji elimu sana kujua kama anachokifanya ni sawa.

"Tundu Lissu anavyoviongea hata mtoto mdogo anajua ni vya uongo, anasema alivyopata matatizo yale hakuna kiongozi wa serikali aliyeeenda kumuona lakini picha zinaonyesha Makamu wa Rais alienda kumuona akiwa Hospitali," alisema Bi. Sara.

"Inaonekana Tundu Lissu bado anaumwa ngoja niseme suala la Tundu Lissu halihitaji elimu sana kujua Tundu Lissu anachokifanya ni sawa."