Malima ashangazwa na Mkude




Mchezaji wa zamani wa Yanga, Simba na Taifa Stars, Bakali Malima amemtaka mchezaji wa Simba SC Jonas Mkude kujiengua katika soka la Tanzania ili kwenda kimataifa zaidi.

Kwa mujibu wa Radio One Malima amesema kuwa ni wakati mwafaka wa Mkude kucheza soka la kimataifa kutokana na uwezo wake Uwanjani.

Malima ameonesha kushangazwa na Mkude kwanini mpaka leo anachezea Simba na ilihali kwa uwezo alionao uwanjani anapaswa kucheza soka la kimataifa.

"Unajua nashangaa mpaka sasa Mkude yupo hapa nchini, muda unaenda na ni wakati wake sasa kucheza soka la kimataifa kwani ana uwezo wa hali ya juu" alisema.

Mchezaji huyo amesema hayo mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likipachikwa na Meddie Kagere.