https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mawaziri saba wakutana Dodoma, wafanya kikao kizito | Muungwana BLOG

Mawaziri saba wakutana Dodoma, wafanya kikao kizito


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi leo tameongoza kikao cha Mawaziri wenzake sita kujadili changamoto mbalimbali za matumizi ya sekta ya ardhi.

Mkutano huo unaohusisha pia Makatibu Wakuu wa Wizara hizo unafuatia maagizo yaliyotolewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli januari 15, 2019 kwa wizara hizo kukutana na kushughulikia changamoto katika matumizi ya sekta ya ardhi kwa nia ya kutatua migogoro.

Mawaziri wanaoshiriki kikao hicho ni kutoka Wizara ya Maliasili na Utaliii, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Maji, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Muungano (Mazingira) pamoja na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kikao hicho cha Mawaziri kimetanguliwa na mfululilizo wa vikao vya timu ya wataalamu kutoka wizara hizo ikioongozwa na Kamishna wa Ardhi nchini Marry Makondo kwa nia ya kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijotokeza katika maeneo mbalimbali nchini.

Muendelezo wa vikao vya aina hiyo ni jitihada za Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha migogoro ya ardhi nchini inapungua kama siyo kuisha kabisa na hivyo kuleta faraja kwa wananchi wanaoishi maeneo yenye migogoro ambao wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi.

Januari 2019 Mawaziri watano wakioongozwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo walikutana mkoani Kigoma kujadili changamoto katika Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba ya Moyowosi mkoani Kigoma. Hifadhi hiyo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu kutokana na wananchi kuendesha shughuli za kiuchumi katika hifadhi hizo.


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa Kikao cha Mawaziri Saba wakioongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kujadili changamoto za sekta ya ardhi nchini.Kikao kimefanyika Ofisi za TAMISEMI Dodoma leo tarehe 7 Februari 2019
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (wa kwanza kushoto) akiongoza kikao kilichohusisha Mawaziri kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Uvuvi na Mifugo, Maji, Wizara ya Maliasili na Utaliii, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Ulinzi, kikao hicho kimefanyika leo tarehe 7 Februari 2019 jijini Dodoma kujadili changamoto za sekta ya ardhi nchini