https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mbunge CCM awashukia CHADEMA kuhusu shambulio la Lissu | Muungwana BLOG

Mbunge CCM awashukia CHADEMA kuhusu shambulio la Lissu


Aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA, Dkt. Godwin Mollel (sasa Mbunge wa CCM, Siha) amesema Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi ni mpango uliosukwa na CHADEMA.

Akizungumza jana Bungeni alisema atathibitisha madai hayo endapo chama hicho kitaeleza walichopanga kuwafanyia Zitto na Chacha Wangwe walipotaka kugombea uenyekiti.

"Mimi nilikuwa huko lakini nilikimbia kwa mipango yao, hata katika tukio la kushambuliwa Lissu mimi niliingia ndani kwenye uchunguzi na niliiba baadhi ya vitu lakini wakakataa mapendekezo yangu," alisema Molllel.

Kwa upande mwingine Mbunge wa Tunduma (CHADEMA), Frank Mwakajoka aliomba taarifa akimtaka Dkt. Mollel kueleza ni kwanini alikuwa anakiuka kiapo cha udaktari, hata hivyo Dkt. Mollel alijibu kuwa alifanya hivyo kwa sababu alikuwa kada mwaminifu wa chama hicho (CHADEMA).