.

2/09/2019

Mbwana Samatta azidi kutisha KRC Genk, atupia kama zote


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa jana ameifungia timu yake, KRC Genk mabao mawili pekee ya ushindi dhidi ya Standard Liege kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A nchini Ubelgiji.

Mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Luminus Arena mjini Genk,Samatta alifunga mabao yake dakika za 67 na 87 na kuifanya timu hicho kuendelea kujimbia kileleni mwa ligi kwa kujikusanyia pointi 57 katika mechi 25 walizocheza

Kwa ushindi huo Samatta amefikisha jumla ya mabao 58 katika mechi 141 za mashindano yote alizoichezea KRC Genk tangu amejiunga nayo January 2016 akitokea TP Mazembe ya DR Congo.