https://monetag.com/?ref_id=TTIb MISA Tanzania yanoa Waandishi Simiyu | Muungwana BLOG

MISA Tanzania yanoa Waandishi Simiyu


Na Clonel Mwegendao.

Wanahabari wametakiwa kuhakikisha wanazingatia haki za binadamu katika kazi zao jambo ambalo litasaidia upatikanaji Wa taarifa zinazozingatia kanuni na sheria ya habari nakuepuka kuandika habari zinazokiuka haki  hizo

Akitoa mafunzo kwa waandishi Wa habari yaliyofanyika Bariadi mkoani Simiyu katika ukumbi wa Sunga kingdom hotel Mkurugenzi mtendaji MISA Tanzania Sengiyumva Gasirigwa amesema kuwa kila Mwandishi anaowajibu Wa kuzijua haki za binadamu ikiwa ni pamoja ni kutambua habari waziandikazo zinagusaje haki za binadamu.

Aidha Sengiyumva ameongeza kuwa haki za binadamu ni zile haki ambazo kila mtu kwa sababu ni mwanadamu anazo ikiwa ni haki za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni ambapo haki hizo zikizingatiwa na kila Mwandishi Wa habari itapunguza uvunjaji Wa haki hizo.

Mkurugenzi  huyo ameendelea kusema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha waandishi wanazijua sheria hizo ikiwemo kueleza changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji kazi pamoja na kupewa ushauli wa kisheria nakujua ni kwa kiasi gani tunafata miiko yetu.

Naye James Marenga ambaye ni mwanasheria na  muwezeshaji (facilitator) katika mafunzo hayo amezitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016,sheria ya haki ya kupata taarifa ya 2016,makosa ya kimtandao ya 2015 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018 pamoja na sheria ya takwimu ni sheria ambazo zimetungwa katika kumuongoza Mwandishi ili kuepukana na changamoto ya utoaji wa habari zisizozingatia vigezo husika vya uandishi.

James ameongeza kuwa mafunzo pamoja na sheria hiyo  itasaidia kufahamu Uhuru wa vyombo vya habari wajibu wetu ni nini,pamoja na kuunda chombo cha waandishi wa habari ambazo watakuwa wamehakikiwa na kufanya kazi kwa uhakika ,kijitengenezea kanuni za uendeshaji wataaluma zao ili kusaidia kuweza kuitwa na kuonywa kwa yeyote atakayekiuka maadili ya uandishi wa habari.

Pia mmoja wa waandishi waliohudhulia mafunzo hayo Dinna Maningo ameeleza changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo ikiwemo kushindwa kuweka wazi baadhi ya habari kutokana na kutokuwa na uelewa dhidi ya haki za binadamu ,mazingira ya kazi,uwezeshwaji wa waandishi kutoka katika vyombo vya katika kufikia urahisi wa upatikanaji wa taarifa

Mafunzo hayo ambayo yameanza leo yameandaliwa na MISA Tanzania na kufadhiliwa na Internews ofisi ya Tanzania yatachukua siku mbili mkoani hapa ambapo tamati yake itakuwa kesho February 17  2018 huku waandishi walioshiriki mafunzo hayo wakitoa matarajio yao baada ya mafunzo hayo ikiwa ni kufanya kazi kwa umahili Mkubwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizofundishwa na kuelezwa katika mafunzo hayo.