.

2/11/2019

Mkurugenzi Itigi kizimbani kwa tuhuma za mauaji


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende (54) na washtakiwa wengine 6 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida leo wakituhumiwa kumuua Isaka Petro.

Wanatuhumiwa kutenda kosa hilo Februari 2 mwaka huu katika Kijiji cha Kazikazi. Upelelezi wa kesi haujakamilika.

Mwanasheria wa serikali Mkuu, Email Kiria amedai kuwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Consolata Singano kuwa February 2, 2019 eneo la genge 48 kijiji cha Kazikazi kata ya Kitakara tarafa ya Itigi, washtakiwa kwa pamoja walimuua Petro.

Hata hivyo washtakiwa hao hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za majuaji, na watendelea kuwa chini ulizi kwa sababu kosa hilo halina dhamana, kesi hiyo itatajwa tena February 25 mwaka huu.