Msanii Godzilla kuzikwa leo Dar


Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Golden Jacob Mbunda a.k.a Godzilla anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Kifo cha msanii huyo kilitangazwa alfajiri ya February 14 mwaka huu taarifa za wauguzi zinaeleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na Malaria.

Taarifa kutoka kwenye familia yake zinaeleza kuwa saa mchana itafanyika misa ya kumuombea kanisa, na baadaye uwanjani (Salasala) kutoa heshima za mwisho, kisha Makaburini (Kinondoni) kwa ajili ya maziko.