Mtanzania, Alice ashinda shindano Benki ya Dunia


Mtanzania, Alice Ahadi Makaga ameshinda shindano la uandishi la kuhusu maendeleo lililoratibiwa na Benki ya Dunia (WB).
.
Alice ambaye kwasasa anasoma mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha African Leadership jijini Kigali ataiwakilisha Tanzania mwezi wa Nne mwaka huu jijini Washington D.C, Marekani kwenye vikao vya WB.

Katika vikao hivyo Alice ataungana na washindi kutoka nchi nyingine, pia kukutana na wadau mbalimbali wa maendeleo. Utakumbuka mwaka 2018 pia Alice alishinda tuzo ya uongozi ya Malkia wa Uingereza.

Tuzo ya Malkia wa Uingereza kwa viongozi vijana hutolewa kila mwaka kama njia moja ya kuitambua kazi inayofanywa na vijana katika jamii mbalimbali za mataifa ya Jumuiya ya Madola, kati ya walioalikwa mwaka huu ni Alice.