Paul Scholes akabidhiwa mikoba ya umeneja

Mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Paul Scholes amepata kibarua cha kuifundisha klabu ya Oldham Athletic inayaoshiriki ligi daraja la pili Uingereza.

Scholes anatarajiwa kutambulishwa rasmi kama meneja wa timu hiyo siku ya Jumatatu mchana na kuanza kazi siku hiyo hiyo.

Katika makubaliano ya meneja huyo na klabu hiyo ameambiwa hatoweza kuruhusiwa kusajili au kuuza mchezaji kwenye timu ya Salford City hii inatokana kwa kua Scholes anasehemu ya umiliki katika timu hiyo.