Picha: Chui Mweusi 'Black Panther' ateka mazungumzo Kenya


Picha ya chui mweusi (black panther) iliyopigwa na mpigapicha Will Burrard-Lucas nchini Kenya imezua gumzo mitandaoni baada ya kudaiwa kuwa ni mara ya kwanza kuonekana katika miaka 100 iliyopita.

Mpinga picha huyo alipata taarifa kuwa chui huyo ameonekana katika kambi ya wanyamapori
ya Laikipia, Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) limeripoti.
Mpiga picha huyo aliamua kuanza kufuatili nyayo za chui huyo kwa kutega kamera maeneo
kadhaa ili kuweza kunasa picha za mnyama huyo.

"Nimezoea kuweka mitego ya kamera na huwa mara nyingine sipate chochote, hujui kama mnyama unayemtaka kumpiga picha atakuja katika njia ulioweka mtego wako wa kamera," ameeleza.
Chui weusi (black panther), jina hilo limepata kuwa maarufu hivi karibuni mara baada ya filamu yenye jina hilo (black panther) kuzinduliwa nchini Marekani na kuweza kuwavutia watazamaji wengi duniani. Tukio la kuonekana chui huyo limekuwa likijadiliwa sana nchini Kenya kwa kile kinachodai ni ki kitu adimu sana na kutokea