.

2/08/2019

Picha: Meli kubwa ya kitalii yawasili nchini


Meli ya kitalii Seabourn Sojourn ikiwa katika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea Zanzibar ikiwa na Watalii wapatao 300. Watalii hao wametembelea mbuga za wanyama, kujivinjari katika fukwe za Bahari ya Hindi, Makumbusho ya Taifa na kituo maarufu duniani cha michoro ya Tingatinga.