.

2/14/2019

Rais Mstaafu Kikwete aumizwa na kifo cha Godzilla


Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ameonyesha kuguswa na kifo cha msanii wa
muziki wa hip hop Bongo, Golden Jacob Mbunda a.k.a Godzilla.

Kifo cha msanii huyo kilitokea alfajiri ya jana, taarifa za wauguzi zinaeleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na Malaria.

"Nimestushwa na taarifa za kifo cha msanii wa kizazi  kipya GodZila. Alikuwa kijana mdogo
mwenye ndoto kubwa na ameondoka wakati ambapo bado mchango wake ulihitajika," ameeleza.

"Nawapa pole familia ya Marehemu na wasanii wote kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze
roho yake mahala pema," ameendika Rais Mstaafu Kikwete kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Godzilla aliugua ghafla majuzi kwa kulalamika anaumwa tumbo na kutapika, alienda kwenye Zahanati ya jirani na kwao, akagundulika ana Malaria. Wakati ameanza matibabu aliendelea kutapika, na kutokula vizuri, hii ikachangia Sukari kupanda na BP kushuka. Mnamo juzi usiku hali ilibadilika ghafla na wanafamilia wakamkimbiza hospitali ya Lugalo ambapo ndio alifariki.