RC Makonda awaandalia viongozi wa dini ziara tatu


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa amewanndalia viongozi wa dini maeneo matatu ya kutalii.

Makonda amesema kuwa viongozi wetu wa dini watakuwa na tour tatu wataenda kuangalia mbuga zetu za wanyama, wataenda kuangalia ujenzi wa Standard gauge na kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

"Kuna ratiba ya viongzi wa dini ambayo tunaiandaa na sio tu mradi huu wa SRG, nina safari pia ya viongozi wa dini ambao niliwaalika Mlimani City lakini wakiwepo na Waislam kumbuka nilifanya mbili za mwezi wa Ramadhan na kipindi cha Christmas kwahiyo tuna tour ya viongozi wa dini tunakwenda Ngorongoro wale wote unaowafahamu tutakuwa na tour yetu ya kwenda kwenye wanyama lakini pia tutakuwa na tour ya kuangalia reli," alisema Makonda alipoenda na wasanii pamoja na waandishi wa habari kuangalia ujenzi wa reli ya Kisasa .

"Kwahiyo viongozi wetu wa dini watakuwa na tour tatu wataenda kuangalia mbuga zetu za wanyama, wataenda kuangalia ujenzi wa Standard gauge na kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)."