RC Mnyeti amcharukia DC suala la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo


Na. John Walter-Manyara

Imeelezwa kwamba Halmashauri ya wilaya ya Hanang Mkoani Manyara imekuwa ya mwisho kimkoa katika zoezi la usambazaji wa vitambulisho maalumu vya wajasiriamali wadogowadogo.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapa,maofisa Tarafa,watendaji wa kata na watendaji wa vijiji wilayani humo ambapo aliwataka watumishi hao kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kazi katika eneo ka kuwagawia wajasiriamali vitambulisha na kwamba atakaekataa afungiwe biashara yake. 

“Zoezi la ugawaji  wa vitambulisho kwa wilaya hiyo hairidhishi kabisa kwani  limeonekana kuwa na kasi ndogo," alisema Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexsander Mnyeti

Kufuatia kusuasua kwa zoezi hilo Mnyeti,alimwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkirikiti kuhakikisha vitambulivyo vya awali alivyopewa 5000 na vingine 6619 alivyomkabidhi viwe vimewafikia walengwa wote ndani ya wiki mbili bila kubaki.

“Ukishindwa kugawa vitambulisho hivyo ndani ya wiki hizo mbili uandike barua ya kujipima ni kwa nini umeshidwa kugawa vitambulisho”alisema mnyeti.

“Inasikitisha ninyi watumishi mkisema kwamba hamna wafanyabishara katika maeneo yenu wakati nyie ndio mliotuletea idadi ya wafanyabishara mlionao,hivyo basi ndani ya wiki mbili kila mmoja awe ameshapatiwa kitambulisho kutokana na idadi mliotuletea”.

Pamoja na kutoa agizo hilo,pia alisema kumekuwa na changamoto ya watendaji kujirahisisha kwa haraka na kujiona hakuna wafanyabisha katika eneo lake anaestahili kupatiwa kitambulisho hicho.

"Nataka kutoa angalizo tu vitambulisho hivi havina uhusiano na ukusaji wa ushuru wa Halmashauri badala yake hupewa kwa mtu kwa biashara yake haizidi milioni 4 na vinadumu kwa mwaka mmoja tu na ambaye hataki kitambulisho mnayo mamalaka ya kumfungia bishara yake,"alisema Mnyeti

Hata hivyo aliwataka maofisa elimu kata kuwaruhusu watumishi hao kutumia pikipiki walizopewa za kata kwa ajili ya kutoa vitambulisho hivyo kwa wajasiriali waliolengwa kupati kitambulisho ili zoezi hilo liweze kumalizika kwa mda huo wa wiki mbili.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Hanang,Joseph Mkirikiti amekiri zoezi hilo kusuasua lakini baada ya kubaini hilo kwa sasa wameanza mkakati wa kupitia duka kwa duka ,waendesha bodaboda,wakulima na wafugaji ambapo mpaka sasa wamekwisha sambaza vitambulisho 2247 kati ya vitambulisho 5000 vya awali walivyopewa.

Wakati huo watendaji hao wakizungumza kwa nyakati tofauti  walisema watahakikisha wanatumia kila njia ili kuweza kuwafikia walengwa wote waliotaja ambao wanastahili kupewa bila kipingamizi chochote.