Saba wanusurika kifungo Tabora


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imewahukumu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja au kulipa faini ya sh. 50000 watuhumiwa saba baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kuingia kwenye hifadhi ya Kigosi Muyowosi iliyopo Wilayani Kaliua Mkoani humo.


Akisoma maelezo ya kosa wakili upande wa Jamuhuri, Tito Mwakalinga ameieleza Mahakama kuwa washitakiwa wote Sabaa walikamatwa na askari wa wanyama Pori ambao Wwlikua wakifanya doria  katika Msitu huo mnamo Tarehe  15 February Mwaka Huu, wakiwa kwenye eneo la Ilindilo  ndani ya hifadhi hiyo ya Kigosi Muyowosi

Mbele ya Hakimu Mkazi mkoa wa Tabora, Joctan Rushwela washitakiwa wote saba wamekili makosa hayo hivyo Mahakama ikawahukumu adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya sh.50000 kila mmoja.

Aidha Watuhumiwa  wote Saba wamenusurika na adhabu ya kwenda jela mwaka mmoja baada ya kulipa faini ya shilingi elfu hamsini kila mmoja.