.

2/14/2019

Shabiki wa Yanga: Kocha wa Simba ana bahati sana


Mwanachama na shabiki wa Yanga SC, Edgar Chibula amefunguka kuwa Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems  alipaswa kufukuzwa kazi kuifundisha timu hiyo.

Shabiki huyo amesema ushindi dhidi ya Al Ahly umemuepusha kuondoshwa akiamini mabosi wake walikuwa wanampigia TIMING tu na angepoteza ingekuwa ndiyo safari yake.

Kwa mujibu wa Radio One, Chibula ameeleza kuwa licha ya kupata matokeo, Aussems angepoteza kibarua chake endapo angetoa sare na kisha kupoteza mchezo ujao wa ligi dhidi ya Yanga.

"Unajua Kocha wa Simba ana bahati sana, ilikuwa ndiyo safari yake endapo angefungwa na Al Ahly Ligi ya Mabingwa Afrika, na kama angebaki, basi Yanga tungemfungashia mizigo yake kwa maana Jumamosi lazima tuchukue pointi 3" alisema Chibula

Mwanachama huyo ameweka jeuri mbele kwa kuamini Yanga itaweza kufanya maajabu kwenye mechi hiyo Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.