.

2/14/2019

Simba SC mbioni kumtangaza kocha msaidizi


Kocha Dennis Kitambi ameeleza kuwa vimebaki vitu vichache vya kumalizana na Simba ili atangazwe kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo.

Simba SC imekaa bila kocha masaidizi tangu klabu hiyo ilipovunja mkataba na Masoud Djuma.

Kitambi tayari yupo kwenye kambi ya kikosi hicho na huenda akaanza majukumu kwenye benchi la ufundi la Simba kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga SC hapo siku ya Jumamosi.

Kocha huyo amewahi kuvinoa vilabu vya Ndanda FC, kocha msaidizi Azam FC na AFC Leopards kutokea nchini Kenya. Dennis Kitambi atakuwa kocha Patrick Aussems ambaye amekiongoza kikosi hicho tangu alipondokaMasoud Djuma.