Simba SC Vs Al Ahly; Viingilio hivi hapa


Homa inazidi kupanda kuelekea pambano la Simba SC na Al Ahly, wenyeweji wa mchezo huo wameweka wazi viingilio vya mchezo huo kwa mashabiki.

Mchezo huo ambao utachezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam February 12 mwaka huu, kiingilio kwa VIP A itakuwa Tsh. 15,000, VIP B Sh. 10,000 na mzunguko Tsh. 2,000.

Simba SC itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kulazwa goli 5-0 na Al Ahly nchini Misri wiki iliyopita.

Hadi sasa Simba SC ina pointi tatu katika michezo mitatu iliyocheza, ikiwa imefunga magoli
matatu pekee, huku ikiruhusu jumla ya magoli 10 katika michezo miwili ya mwisho kucheza dhidi ya AS Vita kutoka DR Congo na Al Ahly.