.

2/11/2019

Wambura asomewa mashtaka 17Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 mawili yakiwa ya utakatishaji fedha.

Wambura amesomewa mashtaka hayo leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza.

Shitaka la kwanza lilikuwa ni kugushi nyaraka wakati akiwa madarakani TFF na kujiwezesha kupata fedha dola 30,000 isivyo halali.

Wambura amekosa dhamana na amepelekwa rumande hadi Februari 14 atakaporejea mahakamani kuendelea na kesi yake ambayo itajulikana iwe ya jinai au uhujumu uchumi.

Itakumbukwa Leo Richrd Wambura ametangaza rasmi kuachana na masuala ya Soka mara baada ya kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa miguu duniani ( TFF).