Wananchi Zimbabwe hatarini kukosa mikate

Wananchi wa Zimbabwe wako hatarini kukosa bidhaa ya mikate kuanzia mwishoni mwa wiki ijayo baada ya Serikali kushindwa kulipia zaidi ya tani 55,000 za ngano iliyokwama nchini Msumbiji huku hazina ya zao hilo iliyopo ni tani 5,800 ambazo zinatosheleza kwa siku 8 tu.

Meneja mkuu wa Chama cha Wasagaji Ngano (GMAZ) nchini humo, Lynette Veremu amekiandiakia barua Chama cha Taifa cha Waokaji Mikate kuwaeleza kuwa tani za ngano zilizopo nchini Zimbabwe ni 5,800 na zitadumu kwa siku 8 tu huku tani 55,000 za ngano zikiwa zimekwama nchini Msumbiji kwakuwa hazijalipiwa.

Mikate ndio chakula cha pili kwa matumizi nchini Zimbabwe ikitanguliwa na mahindi.