Wapinzani wanaleta maneno, wanyamaze na walegee - Mbunge Gekul


Mbunge wa Babati Mjini,  Paulina Gekul amesema kuwa adhma ya serikali ni njema sana ya kugawa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo wadogo huku akisema kuwa ameona wapinzani wakileta maneno hivyo wanyamaze na walegee.

Gekul ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa mtaa wa Osterbay ambapo amesema kuwa watumie fursa waliyopewa na Magufuli katika kupata vitambulisho ili wafanye shughuli zao bila kubugudhiwa.

"Adhma ya serikali ni njema sana kwasababu wenzetu wa upinzani wanaleta maneno, niwaambie wanyamaze na walegee kwasababu hawa watu walikuwa wanateswa sana vyombo vya serikali vilikuwa vinawaonea," alisema Gekul.

"Mh. hataki wafanyakazi wadogo wasumbuliwe amesema chukueni hivi vitambulisho ili mtu akikusumbua katika biashara yako useme nimeruhusiwa na Mh. Rais kitambulisho changu hiki hapa acha kunisumbua," aliongeza.