Watu wanne wafariki kwenye ajali Kagera


Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali ya kugongana kwa magari katika Mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba, Kagera.

Ajali hiyo iliyotokea usiku wa jana February 8,2019 iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 CHC.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema watu wanne wamefariki hadi kufikia sasa.

"Tumeondoa maiti mbili za abiria na dereva mwenye hiyo Hiace pia dereva wa bodaboda aliyekuwa amefunganishwa kwenye hii ajali bahati mbaya amefariki,kwa hiyo jumla ya watu waliofariki katika ajali hii ni watu wanne," amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Maiti zipo hospitali ya Mkoa hazijatambuliwa. Bado tunaendelea na shughuli ya uokoaji na uchunguzi kubaini hasa nini chanzo cha ajali hii na atakayebainika kusababisha ajali,hatua za kisheria zitachukuliwa,'.