https://monetag.com/?ref_id=TTIb Yanga yaipasua Mbao FC | Muungwana BLOG

Yanga yaipasua Mbao FC

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza dhidi ya klabu ya Mbao FC.

Katika mchezo huo Mbao FC ndio walikuwa wakwanza kupata bao kupitia kwa Ndaki Robert dakika ya 45 na kwa upande wa Yanga Heritier Makambo aliisawazishia klabu yake dakika ya 50 wakati lile la ushindi lilifungwa na Amis Tambwe dakika ya 68.