Amissi Tambwe apiga hesabu za Ubingwa Yanga SC


Mshabuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe amesema licha ya matokeo mabaya waliyoyapata dhidi ya Lipuli FC, bado wana nafasi ya ubingwa.

Utakumbuka Yanga Jumamosi iliyopita Yanga SC ilichezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Lipuli FC katika mchezo wa ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

“Tunafahamu ugumu wa michezo iliyobaki, hivyo tumejipanga kwa ajili ya michezo mingine inayofuata kuhakikisha hatupotezi ili tufikie malengo yetu.

Hata Yanga imejiweka katika mazingira magumu, kwani kama Simba ikishinda viporo vyake vyote itaiacha Yanga kwa pointi nane, na hata kama ikipoteza viwili, bado itakuwa juu ya vijana hao wa Jangwani.