Binti wa R Kelly amkana baba yake


Siku mbili baada ya R Kelly kuvunja ukimya wake wa mitandaoni kwa kuamua kuweka Clip akiimba kumtakia mtoto wake Heri ya Siku ya kuzaliwa, Joanne Kelly amemjibu na kumkataa Baba yake mzazi.

“Jina langu ni Buku Abi, Sio Joann, sio JoJo wala binti wa mtu fulani, sitambui jina lingine lolote“ Mtoto huyo ameandika kwenye Instastory yake. “Kama sio mtu wangu wa karibu tafadhali niite Buku au Buku Abi tu.

Hivi karibuni R Kelly alikamatwa na kuwekwa ndani baada ya kufunguliwa mashtaka ya kuwatelekeza na kutotoa malezi ya watoto wake.