3/10/2019

BREAKING NEWS: Ndege ya Ethiopia yaanguka, watu 157 wahofiwa kufarikiWatu 157 wanahofiwa kufa baada ya ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ethiopian Airlines iliyokuwa inaelekea Nairobi kutokea nchini Ethiopia kupata ajali na kuanguka leo Machi 10.

Ndege hiyo imeanguka leo asubuhi majira ya saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki  ikiwa na abiria 149 pamoja na wafanyakazi 8. Msemaji wa shirika hilo ambaye hakutowa jina lake  amethibitisha juu ya taarifa hiyo ambapo imetajwa ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Nairobi nchini Kenya. Waziri mkuu wa Ethiopia ameandika katika ukurasa wake wa Twitta leo Jumapili,10.03.2019 ujumbe wa kutoa pole kwa familia za waliofiwa kufuatia ajali hiyo mbaya.Ingawa pia ujumbe huo haukutowa maelezo zaidi.Ujumbe umesema-

''Ofisi ya waziri mkuu kwa niaba ya serikali na wananchi wa Ethiopia tungependa kutowa pole zetu kwa familia zilizopoiteza wapendwa wao waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikielekea Nairobi Kenya asubuhi ya leo''