https://monetag.com/?ref_id=TTIb DC Muro akabidhi mabwawa manne kwa wafugaji | Muungwana BLOG

DC Muro akabidhi mabwawa manne kwa wafugaji


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro amekabidhi Mabwawa manne makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi na kuvuna maji ya Mvua ya Tsh. Milioni thelathini na nane za maji ya mvua ( 38,000,00 ) kwa Viongozi wa kata ya Oldonyosambu ambao wengi wao wanatoka katika maeneo ya Wafugaji kwa ajili ya matumizi yao na mifugo katika Kijiji cha Lemanda.

DC Muro amekabidhi Mabwaya hayo mara baada ya kuyapokea kutoka kwa wadau wa maendeleo Shirika la OIKOS la nchini Italia kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa ( EU ) Pamoja na ushirikiano wa nguvu za ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Arusha.

Awali Mabwawa hayo yalikuwa na uwezo wa kukusanya ma kuhifadhi maji lita milioni sita tu na sasa yamekarabatiwa na kutengenezwa kuweza kumudu kuhifadhi maji lita million 38, pamoja na ujenzi wa Mapalio ya kisasa ya kunyweshea maji mifugo inayotoka katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha.