3/14/2019

Joshua Nassari (CHADEMA) afunguka kuvuliwa Ubunge


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)amesema kuvuliwa kwake Ubunge ni jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za Bunge.

Leo Machi 14, 2019 Nassari kavuliwa ubunge kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge. Hata hivyo, Mbunge huyo amesema hadi sasa hana taarifa rasmi naye ameona taarifa hizo zikisambaa mitandaoni.

Pia ameeleza kuwa Januari 29 mwaka huu aliwasiliana na Ofisi ya Spika na kueleza juu ya kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge.

Saa mbili zilizopita Spika wa Bunge amemvua ubunge Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu ya Bunge mfululizo (mkutano wa 12,13 na 14). Spika, Job Ndugai ameiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifa kuwa jimbo hilo lipo wazi.