https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kocha wa Kagera Sugar awataka wachezaji kucheza mpira kwa malengo | Muungwana BLOG

Kocha wa Kagera Sugar awataka wachezaji kucheza mpira kwa malengo


Na Clavery Christian, Bukoba

Kocha mkuu wa timu ya Kagera mec mexme amewataka wachezaji wa mpira wa miguu kucheza kwa malengo ili kuweza kutimiza ndoto zao na kufikia mafanikio waliyojiwekea kwenye timu yao kwa kuonyesha juhudi na kujituma wawapo uwanjani.

Mexme amesema hayo jana katika uwanja wa kaitaba baada kumaliza mchezo wa kirafiki kati ya Kagera Suger inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara na Umoja Shooting Stars inayoshiri ligi ya mabingwa wa mikoa inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu mkoani katavi ukiwa ni mchezo wa kuweza kuichangia timu hiyo fedha ya kuiwezesha kwenda kushiriki mashindano hayo.

Amesema kuwa wachezaji wengi wamekuwa na tabia ya kupenda kuonekana uwanjani na siyo kucheza kwa malengo yaliyompeleka uwanjani ambapo amewataka kutambua umuhimu wa mchezo na kutumia vema nafasi wanazozipata pindi wanapokuwa uwanjani ili kuonyesha vipaji vyao na kuweza kusonga mbele. Katika mchezo huo timu ya kagera sugar iliibuka kededea kwa kuifunga umoja shooting stars goli 4 kwa 1.