Kocha wa Yanga SC apewa onyo na Manara



Kuelekea mechi ya Simba dhidi ya AS Vita, Ofisa Habari wa Simba SC Haji Manara amemuonya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kukaa karibu na Wakongo ili kuwapa mbinu.

Manara ameongea kimafumbo bila kutaja jina la Zahera akidai kuwa amesalia Dar es Salaam kuwapokea Vita na hajasafiri kwenda Iringa na timu yake.

Manara ameeleza kuwa Kocha huyo amekuwa akizunguka na Vita jijini Dar es Salaam bila kujua kama anapaswa kuwa na majukumu ya kuisaidia timu yake ambayo ina mechi na Lipuli Jumamosi hii huko Iringa.

Ofisa huyo amemuonya Zahera kuwa makini na anachokifanya kwa sababu hii ni mechi ya kimataifa na kitaifa.

"Hii ni mechi ya kitaifa na ya kimataifa tunaiwakilisha nchi, kuna kocha yeye kazi yake imekuwa ni kuzunguka na Vita tu na aliaga anaenda kwao Congo hata Iringa hajaenda.

Aidha ameendelea kusema kuwa hii ni mechi ambayo nchi inajua, Rais anajua, sasa ole wake aendelee kuwaharibia mipango.