3/15/2019

Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea Leo, Timu hizi kushuka dimbani


Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea Leo ambapo timu sita zitashuka Uwanjani kutafuta pointi tatu muhimu kwenye viwanja tofauti.

Mwadui FC watakuwa kazini kumenyana na Stand United Uwanja wa Mwadui Complex, majira ya saa 10:00 jioni.

Tanzania Prisons watakuwa kazini leo kumenyana na JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine, majira ya saa 10:00.

Azam FC watakuwa Chamazi wakimenyana na Singida United Uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00.