https://monetag.com/?ref_id=TTIb Madereva watake wasitake lazima watii sheria | Muungwana BLOG

Madereva watake wasitake lazima watii sheria


Na John Walter-Babati

Mkuu wa  Usalama Barabarani wilaya ya Babati katika mkoa wa Manyara Azizi Ali Mshamu, amesema madereva wa pikipiki au magari Watake au wasitake ni lazima watii sheria za Usalama barabarani ili kuepuka ajali zitokanazo na uzembe.

Akizungumza na Muungwana Blog, amesema katika wilaya ya Babati ajali zimepungua kwa asilimia 3 ukilinganisha na asilimia 12 kipindi kilichopita mwaka 2017  hadi kufika asilimia 9 mwaka 2018 ikiwa ni jitihada za jeshi la polisi kikosi cha usalama bara barani kupitia operesheni maalumu inayojulikana kama 'nyakua nyakua'.

Amesema ajali nyingi zilikuwa zikisababishwa na madereva wasiozingatia sheria na wengine wakikosa mafunzo ambayo jeshi hilo limekuwa likitembea na kutoa elimu kwa madereva,katika vijiwe vya boda boda na shule za msingi na Sekondari.

Ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wanaovunja sheria za bara barani ili kuweza kudhibiti au kumaliza kabisa ajali za Mara kwa Mara.

Akizungumza kuhusu madereva wa piki piki maarufu kama  boda boda  wasiovaa kofia ngumu,amesema katika vijiwe wamechagua kiongozi atakaekua anatoa taarifa kwa jeshi la polisi na kuwachukulia hatua wahusika.

Amesema kutokana na operesheni hiyo ya Nyakua nyakua kuonyesha mabadiliko makubwa kwa maderva wa magari, mpango walionao ni kuihamishia kwa madereva wa piki piki wasiotii sheria.