3/15/2019

Mbowe amtumia ujumbe Edward Lowassa


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema Lowassa kama amerudi nyumbani awaambie wenzake wadumishe Demokrasia na haki za Watanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Es Salaam, Mbowe amesema kuwa wanamtakia kila la kheri.

“Lowassa amesema amerudi nyumbani. Tunamtakia kila la kheri, lakini awaambie hao wenzake wadumishe Demokrasi na haki za Watanzania uraiani, Mahakamani na Magerezani,” amesema Mbowe.