Mtangazaji Ephraim Kibonde kuzikwa leo Dar


Aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde anatarajiwa kuzikwa siku ya leo katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kabla ya hapo kuanzia saa nne na nusu asubuhi ratiba ya ibada, chakula na kuaga mwili zitaanza nyumbani kwao mbezi Beach.

Taarifa za kifo cha Ephraim Kibonde zilitangazwa asubuhi ya Machi 7 mwaka huu ambapo inaelezwa  alianza kusumbuliwa na Presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza ambapo ndipo alipofikwa na mauti.