Loading...

3/15/2019

Mtuhumiwa wa ujambazi afariki akishambuliana na polisi


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Mwinyiheri Nuhu miaka 24 mkazi wa Mvuleni jijiji Dar es salaam aliyetuhumiwa kuwa ni jambazi amefariki dunia wakati anapelekwa hospitali kufuatia tukio la kurushiana risasi na jeshi la polisi wilayani Muheza mkoani Tanga wakiwa katika jaribio la kuvamia duka la mfanyabiashara Ally Nasoro miaka 50 na kufanikiwa kupora Sh. Milioni moja na hatimaye kuingia mtegoni mwa polisi.

Kamanda wa polisi mkoa humo, Edward Bukombe amesema katika tukio hilo marehemu anadaiwa kushirikiana na wenzake watatu ambao majina yao hayakupatikana kwa urahisi baada ya kufanikiwa kutoroka.

Majambazi hao wamekutwa na silaha aina ya shotgan yenye namba za usajili 12185, gobore, risasi mbili, mapanga mawili, simu, kitambulisho cha mpiga kura na ramani ya nyumba hiyo.
Loading...