Nina mpango wa kuondoka Real Madrid - Raphael Varane


Beki wa klabu ya Real Madrid Raphael Varane huwenda akaimwaga klabu hiyo baada ya kuutaarifu uongozi wa kuwa hayuko tayari kuongeza mkataba na anampango wa kuondoka katika klabu hiyo huku mkataba wake wa sasa ukimalizika June 2022.
.
Inaelezwa kuwa Varane amefikia maamuzi hayo kufwatia nafasi yake kuwa finyu katika kikosi cha kwanza msimu huu baada ya ujio wa Eder Militao kutoka FC Porto Beki huyo mwenye miaka 25 alijiunga na Real Madrid 2011 akitokea klabu ya Lens ya Ufaransa na amefanikiwa kutwaa mataji 16 ikiwemo 4 ya Champions Ligi huku akicheza michezo 268 nakufanikiwa kufunga magoli 12.
.