Loading...

3/17/2019

Polisi Shinyanga wadhamiria kujenga vyoo vya kisasa

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simoni Sirro
Jeshi la polisi wilayani Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameanza kijenga vyoo vya kisasa vitakavyotumiwa na mahabusi katika kituo cha polisi cha wilaya hiyo lengo likiwa ni kubadilisha mfumo wa matumizi ya ndoo kwa mahabusu wanapoenda kujisaidia.

Nao baadhi ya wadau wa maendeleo ambao wameshiriki katika kutatua chamgamoto hiyo wamesema changamoto ya ukosefu wa vyoo katika mahabusu za vituo vya polisi bado ni kubwa huku wakichangia mifuko ya saruji,mchanga na nondo kwa ajili ya ujenzi.

Maabusu ya wilaya ya Shinyanga ni miongoni mwa maabusu zinazotumia mfumo wa zamani wa uondoshaji wa kinyesi katika maabusu hzo kwa kutumia ndoo ambapo ujenzi huo utakapokamilika utarahisisha mfumo wa uondoshaji wa majitaka.
Loading...