Polisi wamtia mikononi mtuhumiwa wa mauaji ya watu watatu Uholanzi



Mtuhumiwa wa mauaji ya watu watatu na kujeruhi wengine tisa kwenye jiji la Utrech nchini Uholanzi amekamatwa na polisi.

Taarifa za awali za jeshi hilo zinasema, Gokmen Tanis ambaye ni raia wa Uturuki anadaiwa kufanya shambulizi hilo kutokana na sababu za kifamilia.

Mwendesha mashtaka wa Uholanzi amesema wamewasiliana na ndugu zake ambao wametoa ushahidi kuwa mtuhumiwa huyo alimfyatulia risasi mmoja wa ndugu hao na kumjeruhi kabla ya kuwaua watu wengine watatu.