Rais wetu Magufuli anajali sana wananchi wake - Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akiwajali sana wananchi wake.

Waziri Mkuu ameeleza hayo katika ziara yake Misungwi wilayani Misungwi alipokuwa
akizungumzia suala la wananchi kuunganishiwa huduma ya umeme.

"Rais wetu Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza
kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na Wilaya yenu hii ya Misungwi," ameeleza.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni Tsh. 27,000. Katika hatua nyingine Wilayani humo, Waziri Mkuu amefungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije.