3/11/2019

Rasmi: Zidane arejea Real Madrid


Zinedine Zidane amerejea Real Madrid kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Santiago Solari. Zidane ambaye aliipa Madrid ubingwa wa Ulaya mara tatu mfululizo amesaini mkataba wa miaka mitatu unaomalizika mwaka 2022. Zidane aliachana na Madrid Mei 31, 2018.

Itakumbukwa kuwa Santiago Solari takribani miezi mitano ameshindwa kuipa mafanikio kimchezo timu ya Real Madrid.

Mpaka sasa katika msimamo LA LIGA Timu ya Real Madrid ipo nyuma kwa alama 12 nyuma ya Barcelona.

Solari licha yakushinda Bao 4 - 1 dhidi ya Real Valladolid siku ya Jumapili, kinachomuondoa nikupoteza mchezo dhidi ya Ajax Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.