Loading...

3/17/2019

Rekodi ya Hans Van Der Pluijm yavunjwa Azam FC


Kocha wa muda wa Azam FC, Idd Cheche amevunja rekodi ya Hans Van Der Pluijm kwa kufunga mabao mengi mara mbili zaidi ya Mholanzi huyo kwenye michezo yao minne ya mwanzo.

Cheche  amekusanya jumla ya mabao 16 kwenye michezo minne ambayo ni sawa na wastani wa mabao 4 kwenye kila mchezo ambao wameshuka Uwanjani kwa sasa wakati Pluijm alikusanya mabao 6 kwenye mechi nne za mwanzo.

Cheche alishinda dhidi ya Lyon Uwanja wa Uhuru kwa mabao 3-1, ikiwa ni mchezo wa ligi na akashinda mchezo wa Shirikisho dhidi ya Rhino Rangers Uwanja wa Chamazi mabao 3-0, kabla ya kuinyoosha JKT Tanzania mabao 6-1 na juzi kumaliza kwa Singida United kwa ushindi wa mabao 4-0.

 Pluijm kwenye michezo yake minne ya awali alikusanya jumla ya mabao sita ikiwa ni michezo ya ligi na michezo hiyo ilikuwa dhidi ya Mbeya City 0-2, Ndanda 0-3, Alliance 0-1 na alitoka sare na Lipuli, michezo yote Uwanja wa Chamazi.

Loading...