Sababu ya wachezaji wa AS Vita kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hii


Timu ya AS Vita benchi lake la ufundi jana liligoma wachezaji wao wasiingie kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa sababu wanahofia kuwa na sumu.

Mmoja wa viongozi wa benchi hilo aliyejitambulisha kwa jina la Daktari Noar alisema walikuwa na  uhakika chumba walichoandaliwa kwa ajili ya mapumziko na kubadilishia nguo kuna dawa ambazo ni kwa ajili ya kuwaumiza wachezaji wao.

Wachezaji hao wa AS Vita waliingia na kukaa kwenye korido walionekana wakiwa wamevalia viziba pua na mdomo vyeupe.

“Tuna uhakika chumba hiki kimepulizwa sumu lakini kwa sababu hatuna vipimo ni ngumu kugundua ni aina gani,”alisema Noar.

Alisema tukio kama hilo kufanyika kwao si mara ya kwanza ilishawatokea katika nchi moja kusini, amesema yote hayo ni mbinu za mchezo Kocha wa AS Vita alibaki anaguna na kunungunika.