Simba SC waeleza mbinu waliyotumia kuwafunga Ruvu Shooting.


Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems ameeleza mbinu waliyotumia kuwafunga Ruvu Shooting.

Hapo jana kwenye dimba la uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba SC waliibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

"Jambo kubwa leo ni kushinda. Sikuridhishwa kabisa na kipindi cha kwanza hivyo nikaamua kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili, mabadiliko ambayo yalileta matokeo kipindi cha pili kwa kufunga magoli mawili” amesema Kocha huyo.

Kwa matokeo ya jana Simba SC wanafikisha pointi 51 katika michezo 20 ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) waliyocheza, huku wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.