3/17/2019

Simba SC wapewa pongezi na Serikali


Msemaji Mkuu wa Serikali, Hassan Abbas ametoa pongezi zake kwa klabu ya Simba SC baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pongezi hizo zimekuja kufuatia Simba kuitandika AS Vita ya Congo kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jana.